Habari Kali
Loading...

Warioba ataka wazee kuachia Ngazi Serekalini

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri viongozi wazee na waliokaa madarakani muda mrefu kuacha kung’ang’ania madaraka.
Amesema kuwa ni vyema kwa viongozi hao kung’atuka ili kutoa nafasi kwa vijana wenye nguvu na akili kulitumikia taifa katika uongozi.
Warioba aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na gazeti hili, pamoja na mambo mengine alizungumzia uongozi wa nchi hii.
“Mwalimu Julius Nyerere aling’atuka akiwa na nguvu zake kabisa. Kiasili kung’atuka ni dhana ya kuwapisha vijana kuwa mbele katika kutekeleza majukumu na ninyi wazee siyo kuondoka, bali kuendelea kuwapa ushauri na mwongozo,”alisema Jaji Warioba.
Alieleza kuwa kung’atuka kunamfanya aliyechukua hatua hiyo kuishi maisha ya raha yenye furaha na amani jambo ambalo yeye sasa analifurahia.
Aliongeza: “Haiwezekani mzee ukakaa kundi moja na kijana wako aliyetahiriwa juzi, kwani kwa kawaida, kijana akitahiriwa hupandishwa daraja na kukaa kundi la wakubwa, hapo wewe baba yake hata kama una miaka 40, unahamishwa na kuingia kundi la wazee.”
jajiwarioba
Alifafanua kuwa hata katika uongozi ni muhimu kung’atuka na kuwapisha vijana ili waweze kutumia akili na nguvu zao kuendeleza taifa huku wakipata maelekezo na mwongozo kutoka kwa wazee.
“Maisha yangu sasa baada ya kuacha uongozi ni ya furaha na amani bila woga kuliko wakati wowote, tofauti na nilipokuwa bado kiongozi katika Serikali,” alisema.
“Ukiwa kiongozi unaweza kuishi kwa hofu na shaka huku ukituhumiwa,” alibainisha Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka 1985 – 1990.
Kauli ya Warioba imekuja huku kukiwa na kundi kubwa la viongozi wenye umri mkubwa katika nafasi mbalimbali madarakani muda mrefu, huku wakiendelea kutamani nafasi za juu zaidi. Miongoni mwa viongozi hao, wapo wanaotajwa kuunda makundi ya kusaka urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Hii siyo mara ya kwanza

Januari 14, 2010, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwashauri wazee watumie busara kupima uamuzi wa kugombea tena nafasi za ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Pinda alitoa rai hiyo alipokuwa akijibu maswali ya wahariri katika mkutano alioitisha kujibu maswali yao jijini Dar es Salaam.
Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania haina tena uhaba wa vijana wasomi na wataalamu wa kuitumikia nchi yao katika nafasi mbalimbali.
“Nafikiri Mkoa wa Rukwa umeonyesha mfano. Mzindakaya na Kimiti wametangaza kung’atuka, nafikiri wazee wengine wafuate busara hiyo,” alisema Pinda.
Dk Chrisant Mzindakaya alikuwa Mbunge wa Kwela na mwenzake, Paul Kimiti alikuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini.
Alisema kuwa rai ya kutaka wazee kung’atuka madarakani ina mambo mawili, ikiwamo kupumzika kwa watu waliokaa madarakani kwa muda mrefu na kwa watu walio na umri mkubwa.
Warioba alisema mtazamo wake ni vyema kuwa na ukomo wa mtu kuwa mbunge, ambapo alipendekeza vipindi vitatu vya miaka mitano mitano yaani miaka 15.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top