Habari Kali
Loading...

POLISI WAFANIKIWA KUMKAMATA MWANAMKE ALIYEKUWA AKIMTESA BINTI YAKE WA KAZI KWA KUMKATA KATA KICHWANI NA KUMG'ATA

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Polisi wamefanikiwa kumnasa mwanamke anayedaiwa kumtesa kwa kipigo na kumng’ata mtoto Merina Mathayo (15), kumsababishia majeraha makubwa kichwani. 
 
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura akizungumza na Mwananchi jana alisema walifanikiwa kumnasa juzi, mwanamke huyo akiwa mafichoni Mbagala wilayani Temeke.
 
“Tumefanikiwa kumnasa juzi usiku akiwa mafichoni kwa jamaa zake, ni mwanasheria wa kujitegemea ana umri wa miaka 44, lakini inashangaza kwa hayo aliyoyatenda, anaendelea kuhojiwa wiki ijayo tunatarajia kumpandisha kizimbani,” alisema Wambura.

 
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Boko, anadaiwa kumtesa mtoto huyo ambaye ni mtumishi wake wa kazi za nyumbani, ambaye sasa amelazwa katika wodi ya dharura ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI) Muhimbili Dar es Salaam.

 
Wakati huo huo, Uongozi wa MOI umejizatiti kulinda usalama wa mtoto huyo, kwa kuzuia vyakula kutoka nje ya taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kudhibiti watu kumtembelea na kuzungumza naye.

 
Mmoja wa wauguzi katika wodi aliyolazwa alieleza mtoto huyo kwa sasa anahudumiwa kila kitu na taasisi hiyo.

 
Ofisa Uhusiano wa MOI, Patric Mvungi , alieleza kwamba majibu ya kipimo kikubwa cha CT Scan alichofanyiwa yametoka, ambapo yameonyesha hakuna mfupa uliovunjika kichwani.

 
Mtoto Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ya kung’atwa meno na kupigwa na vitu mbalimbali.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top