Dar es Salaam.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imefungua milango kwa mawaziri na wabunge kufunguliwa mashtaka kutokana na kauli watakazozitoa bungeni ambazo ni kinyume cha Katiba na Sheria.
Mahakama Kuu ilitoa msimamo huo jana wakati ikitoa uamuzi wa
pingamizi la awali katika kesi ya kikatiba iliyokuwa ikimkabili Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, lililowasilishwa na Jopo la Mawakili wa Serikali
wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG, George Masaju.
Kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013 ilifunguliwa na Kituo cha Msaada wa
Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS), dhidi ya Pinda na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), aliyeunganishwa kama mlalamikiwa wa pili.
LHRC na TLS walikuwa wakidai kuwa Pinda alivunja Katiba kutokana na
kauli aliyoitoa bungeni, wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji
wa sheria kuwapiga wananchi wakati wa vurugu.
Hivyo, walikuwa wakiiomba mahakama, pamoja na mambo mengine, itamke
kuwa kauli hiyo ni kinyume cha Katiba na imwamuru Pinda aifute
hadharani.
Hata hivyo, Pinda na AG waliokuwa wakitetewa na DAG Masaju
akisaidiana na Mawakili wa Serikali Wakuu (PSA, Gabriel Malata, Alecia
Mbuya na Sarah Mwipopo), waliweka pingamizi la awali dhidi ya kesi hiyo,
wakitoa hoja tano za kuomba kesi hiyo itupiliwe mbali.
Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na kwamba kesi hiyo ni batili na iko
mahakamani isivyo halali kwa kuwa inakiuka Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ya Mwaka 1977 na Sheria ya Mamlaka, Kinga na Haki za Wabunge,
ya mwaka 1988.
Mawakili hao walidai kuwa Pinda analindwa na Katiba Ibara ya 100 (1)
na (2), ambazo zinamkinga mbunge kushtakiwa au kufunguliwa shauri la
madai mahakamani kwa jambo lolote alilolisema, au alilolitenda, au
alililoliwasilisha bungeni kwa njia ya maombi, muswada au hoja.
Mahakama Kuu katika uamuzi wake jana ilikubaliana na baadhi ya hoja
za mawakili wa utetezi (Serikali) na kuitupilia mbali kesi hiyo, lakini
ikatamka kuwa wabunge na mawaziri wanaweza kushtakiwa kwa kauli au jambo
walilolitamka bungeni, linalokiuka sheria na haki za binadamu.
Uamuzi huo ulisomwa na Kiongozi wa Jopo la Majaji wa Mahakama Kuu,
lililokuwa likisikiliza kesi hiyo, Jaji Kiongozi Fakih Jundu kwa niaba
ya majaji wenzake, Agustine Mwarija na Dk Fauz Twaib.
Katika uamuzi huo, majaji walikubaliana na hoja tatu za pingamizi
kuwa walalamikaji katika kesi hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi
hiyo na kwamba walikosea taratibu za ufunguaji wa kesi kama hizo kwa
kuwa walikiuka amri na kanuni zinazoongoza Mashauri ya Madai (CPC).
Katika hoja ya kwanza kuwa Pinda kama mbunge analindwa na Katiba,
jopo hilo lilisema kuwa ni kweli wabunge wanalindwa na Katiba Ibara ya
100 (1) kuhusu haki na upendeleo (Previledge), yaani haki na uhuru wa
mjadala na maoni. Hata hivyo, lilikataa hoja za utetezi kuwa wabunge
wana kinga isiyo na mipaka ya kutokushtakiwa kwa kauli au jambo lolote
walilolitamka bungeni.
Badala yake jopo hilo lilikubaliana na hoja za mawakili wa
walalamikaji, kuwa japo wabunge wana kinga, lakini kinga yao ina mipaka
na kwa kuwa inadhibitiwa na masharti ya ibara nyingine za Katiba na
Sheria za Bunge.
Walalamikaji walikuwa wakitetewa na Peter Kibatala, Fulgence Massawe, Harold Sungusia, Mpale Mpoki na Jeremiah Mtobesya.
Kuhusu hoja ya pingamizi kuwa walalamikaji hawakuwa na haki ya
kufungua kesi hiyo, mahakama ilikubali kuwa kwa walalamikaji katika kesi
hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo.
Ilifafanua kuwa anayepaswa kufungua kesi ni yule tu aliyeathirika na
kauli iliyotolewa na mlalamikiwa na si mashirika, kwa kuwa kauli ya
mlalamikiwa haikuyaathiri mashirika hayo yaliyofungua kesi.

Mahakama ilifafanua kuwa mtu aliyeathirika na kauli iliyotolewa
bungeni anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge hasa kanuni ya 71 (1) .
Ilisema kwa kuwa kanuni hiyo haitoi nafasi kwa mashirika, basi
mashirika yanaweza kufungua kesi mahakamani kwa kufuata taratibu za
kisheria, ikiwa kauli iliyotolewa bungeni itakuwa imeyaathiri moja kwa
moja.
Akizungumzia uamuzi huo, Wakili Kibatala alisema kuwa ingawa kesi yao
imetupiliwa mbali, lakini kitendo cha mahakama kutamka kuwa wabunge
hawana kinga isiyo na mpaka na kwamba wanaweza kushtakiwa ni ushindi
mkubwa.
Kwa upande wake Wakili Sungusia alisema kuwa wiki ijayo watakutana na
jopo la mawakili ili kujadili uamuzi huo na hatua za kuchukua kama
watakata rufaa Mahakama ya Rufani au la.
Katika pingamizi lao, mawakili wa utetezi pia walidai kuwa hati ya
madai iliyowasilishwa mahakamani haijasainiwa kwa kuwa waliosaini si
walalamikaji na kwamba hawajaonyesha kama wamepewa mamlaka ya kusaini
kwa niaba ya walalamikaji.
Walidai kuwa walalamikaji ni taasisi yaani LHRC na TLS, lakini
waliosaini ni Dk Hellen Kijo Bisimba kwa niaba ya LHRC na Wakili Francis
Stolla (Rais wa TLS) kwa niaba ya TLS, lakini hawaonyeshi kama wamepewa
mamlaka ya kusaini hati hiyo.
Pia mawakili wa walalamikaji walidai kuwa hati ya madai ina dosari za
kisheria kwa kuwa kwa mujibu wa kanuni za Uendeshaji wa Mashauri ya
Madai (CPC), hati inapaswa kueleza madai tu na si ushahidi, hoja wala
maoni, walalamikaji wameelezea na maoni yao binafsi.
Upande wa walalamikaji katika majibu yao walidai kuwa walalamikaji
wana haki ya kuwashtaki walalamikiwa. Wanadai kuwa kinga ya mbunge ina
mpaka na inamlinda kwa shughuli za bunge tu na kwamba hati hiyo haina
dosari huku wakidai kuwa hata kama zipo dosari za kisheria, basi
zinaweza kurekebishwa.
Pinda alitoa kauli hiyo inayolalamikiwa, katika mkutano wa 11 wa
Bunge wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu
bungeni, Juni 20, 2013.
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM),
Murtaza Mangungu kuhusu msimamo wa Serikali, pamoja na mambo mengine,
malalamiko dhidi ya vyombo vya dola katika baadhi ya maeneo kama Mtwara,
kuwapiga wananchi.
“Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa
tu… Eeh, hamna namna nyingine, eeh maana lazima tukubaliane kwamba nchi
hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi… wewe
ndiyo jeuri zaidi… watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu, kwa sababu
hakuna namna nyingine, eeh… maana tumechoka,” inasomeka hati ya madai
ikinukuu maneno ya PindBONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >