Habari Kali
Loading...

HISPANIA YAPATA KIPIGO CHA KARNE

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== > RIO DE JANEIRO, Brazil
INAWEZEKANA usiamini kilichotokea, hiyo ni kama hukupata nafasi ya kuuona mchezo kati ya Hispania ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, dhidi ya Uholanzi, jana, ambapo mabingwa hao walipata kipigo kikali na cha aibu.
Robin van Persie alifunga bao zuri la kichwa cha umbali wa mita 30 na kuisawazisha Uholanzi dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza.
Uholanzi ikicheza kwa kujiamini, kushambulia na mpira wa kasi ilifanikiwa kuifunga Hispania mabao 5-1 katika mechi ya Kundi B kwenye michuano ya Kombe la Dunia ndani ya Dimba la Nova.
Robin van Persie na Arjen Robben wakipongezana.
Hispania ndiyo iliyoanza kufungua ukurasa wa mabao kwa kufunga katika dakika ya 27 kupitia kwa Xabi Alonso kwa penalti iliyotokana na straika wa Hispania, Diego Costa kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Uholanzi ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kupitia kwa Robin van Persie ambaye alifunga bao kali kwa kichwa huku akimuacha kipa wa Hispania, Iker Casillas akiwa hana la kufanya.
Mwanaume kazini.
Mabao matatu yaliyopatikana katika dakika ya 53 kupitia kwa Arjen Robben, Stefan de Vrij dakika ya 64, van Persie tena katika dakika ya 73 ambapo bao hilo lilitokana na uzembe wa Cassillas ambaye alishindwa kuucheza mpira aliorudishiwa, Robben tena dakika ya 80 yalitosha kuwamaliza nguvu Hispania, ndipo wakakubali kipigo hicho mpaka mwisho wa mchezo.
 Robin van Persie akimlamba chenga kipa wa Hispania, Iker Casillas kabla ya kuifungia Uholanzi bao la nne katika ushindi wa 5-1 kwenye mechi ya Kundi B Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Cameroon Vs Mexico
Mexico ambayo ilikuwa na staa wa Manchester United, Javier Hernandez ‘Chicharito’ ilipata bao lake pekee kupitia kwa Oribe Peralta ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Giovani dos Santos katika dakika ya 61.
Dos Santos alipiga shuti kali baada ya kuwatoka mabeki wa Cameroon iliyokuwa ikiongozwa na straika mkongwe wa Chelsea, Samuel Eto’o, ambapo kipa Charles Itandje akalipangua, ndipo Peralta akamalizia.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top