Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetangaza
kuhamisha kituo maarufu cha daladala cha Mwenge kwenda eneo la
Makumbusho.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ofisa mfawidhi wa Sumatra wa
Kanda ya Mashariki, Conrad Shio alisema Kituo cha Mwenge kitafungwa
rasmi Jumapili na eneo hilo litabaki wazi kupisha upanuzi wa Barabara ya
Ali Hassan Mwinyi. Shio alieleza sababu ya kuhamisha kituo hicho kuwa
ni ufinyu wa eneo lenyewe jambo linalosababisha magari kushindwa kuingia
kituoni hapo kwa wakati, hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hiyo
husababisha foleni kubwa isiyo ya lazima.

Alisisitiza madereva wote kutii agizo hilo kuanzia Jumatatu na kwamba atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, aliwataka abiria kutolazimisha kushushwa katika eneo hilo wakati hakuna kituo. Shio aliongeza kuwa barabara za kuingia na kutoka Kituo cha Makumbusho bado zinakarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa magari katika kituo hicho.
Hivi karibuni, madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mwenge, Tegeta na Ubungo waligoma kutoa huduma kushinikiza Serikali kueleza kituo mbadala baada ya kufungwa kwa kituo cha Ubungo kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

