Habari Kali
Loading...

Sheikh Ponda agoma kwenda mahakamani,achoshwa na tabia ya kuhairishiwa kesi yake mara kwa mara…!!

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== > Kiongozi wa Taasisi ya Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aligoma kufikishwa mahakamani kutoka mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Morogoro, akidai kuchoshwa kuhairishwa kwa kesi yake kila anapofikishwa mahakamani.
Pamoja na kuchelewa kufikishwa mahakamani, kesi yake iliahirishwa tena hadi Juni 10 baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo kusema kuwa jalada bado halijarudishwa kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
sheikh ponda
Wakili wa kiongozi huyo, Bathelomeo Tarimo alilalamikia hali hiyo na kutaka haki itendeke kwa mteja wake.
Akizungumza jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema kuwa kukwama kwa faili la Sheikh Ponda ni kutokana na maombi namba 25 ya mwaka 2014 yanayosubiri kusikilizwa mahakamani hadi sasa.
Msajili alisema kuwa maombi ya Sheikh Ponda ya kutaka kuharakisha usomaji wa rufaa ili utolewe uamuzi na kesi hiyo kumalizika au kuendelea, yatasikilizwa na Jaji Lawrence Kaduri, Juni 16.
Kwa upande wake, Wakili Tarimo alidai kuahirishwa kwa kesi hiyo kunatokana na kucheleweshwa kusomwa kwa rufani yake namba 89 ya mwaka 2013 aliyowasilisha Mahakama Kuu Septemba 14 mwaka 2013.
Wakili Tarimo alidai kuwa, rufaa hiyo inahusu moja ya shtaka linalomkabili Sheikh Ponda lililotokana na uamuzi uliotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Alidai kuwa majalada yote yanayohusu kesi ya Sheikh Ponda yapo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lakini cha kushangaza kesi imekuwa ikiahirishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, jambo ambalo alidai kuwa limeanza kumtia wasiwasi mteja wake.
Upande wa Jamhuri unaowakilishwa na Wakili Sunday Hyera uliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi na kupanga tarehe nyingine ya kutajwa wakati jalada halisi la kesi hiyo lililoitishwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, likiendelea kusubiriwa kuletwa kortini.

Credit: Mwananchi

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top