Habari Kali
Loading...

MTOTO ACHOMWA MOTO NA BIBI YAKE BAADA YA KUIBA KARANGA ZA BIBI HUYO HUKO GEITA

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Mwanafunzi wa darasa la tatu Sofia Damasi (12) wa shule ya msingi Lutozo katika kata ya Katoro wilayani Geita mkoani Geita amelazwa katika kituo cha afya mjini Katoro baada ya kuchomwa  moto sehemu mbalimbali za mwili wake na bibi yake.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 8 katika kitongoji cha Bulengahasi.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa bibi huyo anayeitwa Monica Petro(50) ambaye ni mkazi wa Katoro aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya mjukuu wake huyo kumwibia karanga za mbegu alizokuwa amezitunza kwa ajili ya kupanda.

Akiongea kwa shida alikolazwa wodi ya wanawake mtoto huyo amesema kuwa alikumbwa na mkasa huo juzi majira ya saa 8 mchana muda mfupi baada ya kumaliza kula chakula cha mchana.

“Baada ya kumaliza kula chakula bibi yangu alitoka nikabaki mimi nyumbani na baba zangu wadogo wawili ambao nao baadaye waliondoka na kwenda kazini kwao na ndipo bibi yangu alirudi tena na kuingia jikoni’’,alieleza.

“Bibi alipoingia jikoni aliniita jikoni na nilipoenda jikoni bibi yangu alifunga mlango kwa ndani na kisha kunifunga kamba aina ya mpira mikononi mwangu na kuanza kunitesa’’alifafanua mtoto huyo/

Alisema mara baada ya kufanya unyama huo bibi yake alitoka nje na kumfungia ndani na ndipo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada ndipo majirani walifika na kumfungulia mlango na kamba hiyo na baada ya hapo walimpeleka kituo cha polisi na kupewa hati namba tatu ya matibabu(PF3) kwa ajili ya kupata matibabu na kisha kupelekwa kituo cha afya cha Katoro.


Afisa mtendaji wa kata ya katoroAloyce Kamuli alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema  hana taarifa kuhusu tukio hilo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top