Moja kati ya maadui wakubwa wa usingizi ni mdudu ‘kunguni’ ambaye
anaweza kumfanya mtu anayepanga kujipumzisha kuhisi anaadhibiwa kwa
kufinywa.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Pugu iliyoko Dar es Salaam,
ambayo ina historia ya pekee kwa kuwa ni moja kati ya shule
alizofundisha muasisi wa Taifa hili, mwalimu Julius Kambarage Nyerere
wamekumbwa na mtihani mkubwa na kulazimika kuyakimbia mabweni yao
kutokana na kushambuliwa vikali na mdudu aina ya ‘kunguni’.
Kilio cha wanafunzi hao wa shule hiyo ya bweni inayochukua
wanafunzi wa kiume pekee kimeripotiwa na Edson Mkisi Jr, mtangazaji wa
kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm aliyetembelea shule hiyo.
Mkisi alipata nafasi ya kuongea na baadhi ya wanafunzi wa shule
hiyo ambao walieleza hali ilivyo na kwamba kwa jinsi ambavyo
wanaongezeka, imewabidi watumie muda mwingi kuwa madarasani hata nyakati
za usiku na hata kulala huko.
Hali inayowafanya washindwe kupumzika vizuri na kuathirika kwa kiasi kikubwa kimasomo.
Nae Makamu Mkuu wa shule ya Pugu, amethibisha kuwepo kwa tatizo
hilo na kwamba tayari uongozi wa shule hiyo umemuomba msaada meya wa
Ilala, Jerry Slaa ili waweze kusaidiwa kuwatokomeza wadudu hao na
ameahidi kuwasaidia.
Hata hivyo, wanafunzi hao wamekiri kuwa kumekuwepo na jitihada za
kutosha zinazofanywa na wanafunzi na walimu katika kupambana na wadudu
hao lakini wadudu hao hutoweka kwa muda na kurudi tena hasa kipindi cha
joto.
Uamuazi wa wanafunzi hao kulala madarasani ni hatari zaidi kwa
kuzingatia tishio la ugonjwa hatari wa Dengue unalolikabili jiji la Dar
es Salaam, unaoambukizwa kwa kuumwa na mbu.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

