JESHI la
Wanachi wa Tanzania (JWTZ), limeonya kuwa liko imara na litaendelea
kusimamia na kutii amri na maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya
Kikwete.
Pia, limesema kamwe halitayumbishwa na hila na kauli za kisiasa zinazotolewa kwenye majukwaa.
Kauli hiyo ya
wapiganaji na walinzi wa taifa ilitolewa bungeni jana na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, wakati
akiwasilisha Makadirio ya Matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Alisema Rais
Kikwete ni kiongozi shupavu, mvumilivu na mwenye kupenda maridhiano,
mambo ambayo yatamfanya akumbukwe na kuenziwa vizazi na vizazi.
“Ahadi yetu
kwake ni kuwa tutaendelea kusimama imara kupokea na kutii amri na
maelekezo yake bila hila yoyote na kutoyumbishwa na kauli potofu za
kisiasa,’’ alisema Dk. Mwinyi.
Alisema katika
kipindi cha mwaka 2014/2015, wizara inakusudia kuimarisha utendaji kazi
na ufanisi wa jeshi hilo katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa taifa
kulingana na dira, dhima na malengo.
‘’Mpango wa
ununuzi wa zana za kisasa na bora za kijeshi ni endelevu, hivyo
natarajia Bunge lako litaendelea kuidhinisha na kutekeleza mpango huu,’’
alisema.
Alisema mpango huo unalenga kuimarisha mafunzo ya kijeshi kwa vijana kwa mujibu wa sheria na wale wa kujitolea.
Dk. Mwinyi
alisema mpango huo unalenga kununua vifaa na zana za kijeshi za kisasa,
vikiwemo vifaa vya uhandisi wa medani na ndege za kivita na kuendelea na
ujenzi wa nyumba 6,064 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi.
Aidha alisema
hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vimeanza kutekeleza utaratibu wa
kuajiri vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa.
Alisema katika
kipindi cha mwaka huu, vijana 7,062 waliajiriwa na vyombo hivyo huku
wengine 155 wakichukuliwa na kampuni binafsi, ikiwemo Benki Kuu, Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege na Kampuni za Madini za Barrick na Geita Gold
Mines.
Alisema kwa kipindi cha mwaka huu, vijana 45,000 watakaomaliza kidato cha sita watachukuliwa kwa ajili ya mafunzo ya JKT.
Mwinyi alisema utaratibu wa vijana waliomaliza kidato cha sita kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria si wa hiari.
Akizungumzia uvamizi wa maeneo ya jeshi, Dk. Mwinyi alisema tatizo hilo bado kubwa na linaendelea.
Alisema katika
kipinchi hiki, maeneo yaliyoathirika na tatizo hilo ni pamoja na
Tondoroni (Pwani), Tanganyika Packers na Monduli (Arusha), Kimbiji (Dar es Salaam), Chita (Morogoro), Itaka na Uyole (Mbeya).
Sehemu nyingine ni Uwanja wa Ndege na Ilemela (Mwanza) na Kisakasaka (Unguja).
>>Gazeti la Uhuru
>>Gazeti la Uhuru
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


