Lanjui aliyekuwa dereva wa taasisi aliyoiita “Mamlaka ya Pamba,”
alipata ajali hiyo mkoani Mwanza baada ya lori alilokuwa akiendesha
kuchomoka gurudumu la mbele na kupinduka.
“Sababu ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni ajali
iliyosababisha kupooza kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo. Kwa kuwa
sinyanyuki kitandani, nimepata vidonda kuanzia makalioni hadi miguuni.
Kwa sasa naishi maisha magumu mno,” alisema.
Aomba msaada
Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali na jamii kwa jumla kumsaidia
chakula kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia. Lanjui ambaye hawezi
kunyanyuka kitandani, alisema kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya
mkoa ulikuwa ukimhudumia kwa kumpa chakula lakini baadaye huduma hiyo
ilisitishwa, hivyo kumfanya awe ombaomba na maisha yake kuwa ya mlo
mmoja kwa siku.
“Kwa vile siwezi kunyanyuka kitandani na sina ndugu yeyote, nimekuwa
nikiwaomba msaada manesi na watumishi wengine wa hapa hospitali.
Nashukuru sana wamekuwa wakinisaidia bila kuchoka na kuniwezesha kupata
walau mlo wa siku moja,” alisema. Lanjui ambaye anazungumza vizuri pia
aliomba msaada wa fedha za kwenda Hospitali ya KCMC, Moshi ili apatiwe
huduma zaidi ya matibabu.
Mwanza hadi Singida
Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu
Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure,
Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.
Alisema akiwa Sekou Toure mwishoni mwa mwaka 1970, hali yake
ilibadilika na kuwa mbaya ndipo alipomwomba mwajiri wake amrudishe
nyumbani katika Kijiji cha Mhintiri katika Wilaya ya Ikungi mkoani
Singida ili ‘akasubiri kifo chake.’
Hata hivyo, alisema uongozi wa Mamlaka ya Pamba ulikataa kumpeleka
kijijini kwake, badala yake ulimkabidhi katika Hospitali ya Mkoa wa
Singida mwaka 1971.
Alisema wakati anapata ajali na kulazwa hospitalini, wazazi na ndugu yake wa pekee, walikuwa wamekwishafariki dunia.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Mussa Kamala alisema hivi sasa mgonjwa huyo anahudumiwa na hospitali kama watu wengine wenye ulemavu ambao hawatozwi gharama yoyote.
Alisema uongozi wa hospitali uliwahi kumkabidhi kwa Idara ya Ustawi wa Jamii ili ifanye mipango ya kumrudisha nyumbani, lakini haikuwezekana. Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida, Zuhura Kalya alisema walishindwa kumrejesha kwao kwani walipofuatilia ilibainika kuwa hana ndugu na hakukuwa na mtu anayemfahamu kwa sababu aliondoka kijijini hapo mwaka mmoja baada ya uhuru.
Alisema uongozi wa hospitali uliwahi kumkabidhi kwa Idara ya Ustawi wa Jamii ili ifanye mipango ya kumrudisha nyumbani, lakini haikuwezekana. Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida, Zuhura Kalya alisema walishindwa kumrejesha kwao kwani walipofuatilia ilibainika kuwa hana ndugu na hakukuwa na mtu anayemfahamu kwa sababu aliondoka kijijini hapo mwaka mmoja baada ya uhuru.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

