Watu watatu wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini
Zanzibar baada ya kushukiwa kuwa na maradhi ya homa ya Dengue
inayosababishwa na mbu aina ya “Aedes”.
Ugonjwa huo tayari umeingia jijini Dar es Salaam na kuathiri watu zaidi ya 400 huku wengine wakiripotiwa kufariki.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, Waziri wa Afya,
Juma Duni Haji, alisema, wagonjwa hao wametokea katika maeneo ya vijiji
vya Kama na Mwera.
Alisema, tokea wagonjwa hao wabainike, uongozi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja umeamua kuchukua vipimo kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi
zaidi, ikiwa ni hatua ya kuweza kupata uthibitisho wa wagonjwa hao kama
wanaugua homa hiyo.
“Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kuchukua hatua mbalimbali
ikiwemo kuchukua vipimo (Sample) ili kuchunguza kuwepo kwa virusi hivyo
na kufuatilia sehemu walikotoka wagonjwa ili kutathmini hali halisi ya
mazingira”, alisema Waziri huyo.
Waziri Duni, alisema, wanalazimika kuchukua hatua hiyo kwa vile
maradhi hayo ni mara ya kwanza kujitokeza hapa Zanzibar, hivyo ni vyema
wananchi wakaona umuhimu wa kusafisha mazingira yanayowazunguka.
Aidha, alifahamisha kuwa hadi sasa hakuna tiba maalum ya ugonjwa
huo, na kwamba mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana
kama vile homa, kupungukiwa na maji au damu huku akisisitiza hakuna
chanjo kwa ajili ya kinga.
Waziri Duni, alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo, serikali
hivi sasa, inawasiliana na mashirika mbalimbali ya kimataifa ili yaweze
kuwasaidia katika kuleta vifaa vya uuguzi kwa wagonjwa watakaopatwa na
tatizo hilo.
Aliyataja mashirika ambayo wameanza kuwasiliana nayo ni pamoja na WHO, NIMR na Wizara ya Afya Tanzania Bara.
Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa
habari juu ya hofu ya kuwepo kwa wagonjwa watatu wanaoshakiwa kuwa na
dalili za ugonjwa wa Dengue.
Alizitaja dalili za ugonjwa huo ni homa ya hafla,mwili kuchoka,
kuumwa na viungo, kuvimba tenzi na kupatwa na haraha (Vipele), kuumwa na
kichwa ambapo dalili zake huanza kujitokeza kuanzia kati ya siku tatu
na 14 tangu mtu alipoambukizwa.
“Dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za
malaria na homa ya mafua, hivyo nawaomba wananchi kuwa waangalifu hasa
wakati wanapopata homa ambazo zinafanana na malaria kukimbilia vituo vya
afya,” alisema.
Hata hivyo, alifahamisha kuwa kuna aina tofauti za ugonjwa huo, ikiwemo (Dengue Fever) ambapo huambatana na dalili kuu tatu za homa kali ghafla, kuumwa kichwa na maumivu ya viungo au uchovu.
Dk. Salma Masauni Yussuf, ambae ni Mkuu wa Kitengo
cha kuzuia na kudhibiti maradhi Zanzibar, aliwataka wananchi
kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha hali inakuwa nzuri hapa nchini
huku akiwanasahi kusafisha mazingira hasa katika kipindi hichi cha mvua
za masika zinazoendelea.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

