Habari Kali
Loading...

BAADA KUMTUNDIKA MIMBA MSANII MWENIZIE:NEY WA MITEGO NDIYE CHANZAO CHA KUVUNJIKA KWA NDOA YA MSANII WA FILAMU "SKAINA" AMBAYO HAIKUDUMU HATA MWEZI

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
SASA hakuna ubishi kuwa, ile ndoa iliyofungwa kwa mbwembwe na kuvunjika kabla ya mwezi mmoja kati ya msanii wa filamu za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na Saad Omar, chanzo ni Mwanabongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’.
Nay wa Mitego 'True Boy'.
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya Skaina iliingia mdudu baada ya mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi kwenye gunia’, kwani bidada huyo alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.

Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7, 2011 nyumbani kwa dada yake, Magomeni – Mapipa, Dar na kufika tamati kabla ya mwezi Novemba, dah!
Ripoti zilizopo kwenye makabrasha ya Risasi Mchanganyiko zinaonesha kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad alimweleza Nay sababu na kutimkia kwao Iringa ambapo alipojifungua alimweleza ukweli mwenzi wake huyo kuhusu ujio wa mtoto wao.
 
Skaina.
Wawili hao wameelezwa kuwa na mawasiliano ya karibu lakini ya siri kwa muda mrefu ila hivi karibuni, wote waliamua kuutua mzigo huo na kuweka mambo hadharani ambapo kwa upande wa Skaina alisema: “Nadhani mmechelewa tu kujua, lakini habari ndiyo hiyo.”
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”

Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi iliyopita, baada ya Nay kutwaa tuzo moja ya Kili katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, Skaina alitupia maneno ya kumpongeza Nay katika ukurasa wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema:
“Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua tuzo, Mungu akuzidishie baraka na maisha marefu ili mwakani uweze kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa sana na kazi zako dady wetu (akimaanisha yeye na mwanaye).”

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top