STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman ameonesha upande wake wa pili baada ya kuwabwatukia wakwe zake aliposikia kuwa wana mpango wa kumpa talaka ili aachane na mumewe Sunday Demonte kutokana na tabia yake kwa kuwa siyo mwanamke wa kuoa (wife material).
Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati jijini Dar, Aunt alidai kuwa alikerwa na jambo hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na kuwawakia kuwa hajaolewa na ndugu hivyo mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba, amekuwa akisikia mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na mumewe.
Alidai naye ni binadamu hivyo jambo hilo limekuwa likimkera kwa sababu wanaongea maneno hayo pembeni na kwamba hakuna hata mmoja aliyewahi kumfuata na kumwambia juu ya suala hilo, zaidi amekuwa akiambiwa na watu wengine tu.
Akifafanua zaidi, Aunt alisema kwamba anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa Demonte kuendelea kumtolea maneno ya kejeli kila kukicha na wakati kama wanahisi kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza kumtafuta na kuzungumza naye.
Alitiririka kuwa jambo ambalo halimpendezi ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka kumpatia talaka.
“Ujue hao ndugu wanaotaka kunipa talaka wanatakiwa waelewe kuwa mimi sijaolewa na wao, hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo lao, maana niko vizuri na mume wangu, wala hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana ishu za kupeana talaka,” alisema Aunt.
Ndoa ya Aunt imekuwa ikisengenywa tangu ilipofungwa mwezi June, 2012 kufutia staa huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye inasemekana anaishi Dubai.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

