Ilijulikanaje kama hakuna kadi?
Chanzo hicho kilimtaja mtoto wa kike wa marehemu Gurumo aitwaye Mariam ambaye anataka nyumba na gari hilo aina ya Toyota FunCargo viuzwe ili watoto wagawane fedha.
“Yule binti alikwenda nyumbani kwa mama yake (mke wa mwisho wa mzee Gurumo aliyekuwa akiishi naye kwenye nyumba yake Mabibo, Dar) na kumtaka ampe kadi ya gari akidai ni la kwake na anataka kuliuza.
“Mama mtu alimwambia mwanaye kuwa baba yao hakupewa kadi hiyo siku alipokabidhiwa gari hilo.
“Hata hivyo, mama huyo alisema siku moja mzee Gurumo alimfuata Diamond alipokuwa akifanya shoo pale Coco Beach (Dar) kwa ajili ya kuulizia kadi hiyo ndipo Diamond akamwambia kwamba akitaka kadi amuulize mtu mmoja aliyesema ni kiongozi mmoja, anafanya kazi maeneo ya Posta Mpya jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa),” kilisema chanzo.
Kukosekana kwa kadi hiyo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa gari hilo, kwani kama ingekuwepo, lingeshauzwa.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Diamond zilisema kuwa tukio la kutoa gari kwa mkongwe huyo mwanzilishi wa Bendi za Mlimani Park Orchestra na Msondo Music Band ulikuwa ni mpango maalum wa kumpromoti msanii huyo ili aweze kung’ara zaidi katika vyombo vya habari ambao uliratibiwa na kiongozi huyo mwenye kulalamikiwa na wasanii mara kwa mara.
Hata kiongozi huyo alipopigiwa simu, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, pia hakujibu.
Mwaka jana Diamond alimpatia mzee Gurumo gari hilo kama sehemu ya kuenzi mchango wake katika muziki wa Tanzania tukio lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar kabla ya mzee huyo kufariki dunia Aprili 13, mwaka huu.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >